Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (AS) - ABNA - , Chombo cha Habari cha Kiebrania kilifichua sababu ya kumwita Waziri Mkuu wa Israel katika Ikulu ya White House kukutana na Rais wa Marekani. Kufuatia matukio yanayohusiana na safari ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu nchini Marekani, Kanali ya 12 ya utawala huo imefichua leo (Jumanne) kwamba, sababu kuu ya kualikwa kwa haraka Waziri Mkuu wa utawala huo Mjini Washington ni uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuanza mazungumzo ya moja kwa moja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wakati huo huo Shirika la Redio na Televisheni la Israel pia lilitangaza kuwa mkutano wa Netanyahu na Trump haukuwa na mashiko.
Kwa mujibu wa ripoti hii, ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Mjini Washington haikuleta mafanikio yoyote yanayoonekana, si katika suala la kupunguza ushuru wa forodha wala katika kuendeleza mazungumzo ya pande mbili.
Shirika hilo pia liliongeza: "Safari iliisha ghafla na kwa kasi isiyo ya kawaida, ambayo baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa ni ishara ya tofauti zilizofichwa au matukio yasiyotarajiwa nyuma ya pazia katika uhusiano kati ya Tel Aviv na Washington."
Benjamin Netanyahu alisafiri hadi Marekani siku ya Jumatatu katika ziara rasmi. Katika safari hii, alikutana na kuzungumza na Donald Trump na kuhitimisha safari yake.
Kuhusiana na hilo gazeti la Kiebrania la "The Times of Israel" liliandika: Ziara ya Waziri Mkuu katika Ikulu ya White House ilikuwa ya kukatisha tamaa kwa sababu Trump alitangaza mazungumzo na Iran.
Gazeti la Al-Akhbar pia limeandika katika dokezo kuhusu suala hili kwamba, wakati utawala wa Kizayuni unakabiliwa na migogoro isiyo na kifani ndani na nje ya nchi, ziara ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu wake nchini Marekani si tu kwamba imeshindwa kutengeneza mwanya wa mahusiano na Washington, bali kuna dalili za kushadidi hitilafu na Serikali ya Marekani katika masuala muhimu, yakiwemo vita vya Ghaza, uhusiano na Iran na ushuru wa kibiashara.
Your Comment